Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

ZAIDI YA WAGONJWA 200 WANUFAIKA NA HUDUMA YA CT-SCAN INAYOPATIKANA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KATAVI

Posted on: February 17th, 2024

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi imefanikiwa kunufaisha Wagonjwa zaidi ya 200 kutokana na uwepo wa huduma ya CT-SCAN ambayo awali huduma hiyo ilikuwa haipatikani Mkoani hapa.

Akitoa ripoti hiyo, Radiografa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Ndg. Martin Misalaba, amesema uwepo wa huduma hiyo umepunguza gharama za wagonjwa kusafiri umbali mrefu kwenda Hospitali zingine kwa ajili ya kupata huduma.

Ndg. Misalaba amesema kuwa Huduma hii tangu ianzishwe imewanufaisha Wagonjwa zaidi ya 200 na imepunguza vifo na gharama za safari kwenda Hospitali zingine kwa ajili ya vipimo.

"Kwasasa tunahudumia wagonjwa wanaotoka wa hapa Katavi na mikoa ya jirani na niwakaribishe Wateja wanaohitaji Huduma hii kwani ipo katika Hospitali yetu muda wote”, amesema Ndg. Martin Misalaba.