Background
Hospital rufaa Mkoa Katavi iko katikati ya mji karibu na kanisa la RC katika kata ya kawajense. Ilianza kama zahanati ya kanisa RC kabla ya kukabidhiwa serikali na kuwa kituo cha afya mwaka 1957.
Hospitali imekuwa ikifanya kazi kama hospitali ya wilaya ya Mpanda hadi Agosti 2016 na kuwa mikononi mwa almashauri ya manispaa na kupewa jina la Hospitali ya Manispaa ya Mpanda. Kisha mnamo Agosti 2017 ikakabidhiwa Wizara ya Afya na kupanda hadhi hadi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi chini uongozi wa mkurugenzi Hospitali.
Kihistoria hospitali ilianza mwaka 1957 kama kituo cha afya wilaya ya Mpanda. Katika kipindi cha mwaka 1977 ilipandishwa hadhi kuwa hospitali ya wilaya. Agosti, 2017 ilipandishwa kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Hospitali ina jumla ya wodi 7 na vitanda 160 kama ifuatavyo; vitanda 16 katika wadi matibabu ya wanaume na vitanda 16 katika wodi ya upasuaji wanaume, vitanda 21 katika wodi ya matibabu wanawake na vitanda 16 katika wodi ya upasuaji wanawake, wodi ya wazazi ina vitanda 37, wodi ya magonjwa ya watoto ina vitanda 30 na wodi ya daraja la kwanza vitanda10