Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

Waziri wa Afya, Mhe. Mhagama akabidhi Tuzo kwa utoaji bora wa huduma kwa Wananchi

Posted on: April 7th, 2025

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Aprili 8, 2025 amekabidhi tuzo na zawadi kwa Mikoa, Wilaya, vijiji na shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu katika utunzaji wa mazingira pamoja na Hospitali za Kanda, Hospitali za wilaya, mikoa, vituo vya afya na zahanati katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Tuzo hizo amezitoa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Katika utoaji wa Tuzo hizo Mhe. Mhagama ameambatana na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi- Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.

Maadhimisho ya Wiki ya Afya yameadhimishwa kwa mara ya kwanza nchini, Yalianza Aprili 3, 2025 na kilele chake ni leo Aprili 8, 2025, yakiwa na kauli mbiu “ Tulipotoka, Tulipo, Tunapoelekea; Tunaijenga Taifa Imara na lenye Afya”.