WAUGUZI NI WATU MUHIMU SANA KATIKA SEKTA YA AFYA, TUTAYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YENU"
Posted on: May 6th, 2025
Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Ndg. Albert G. Msovela amewapongeza Wauguzi
wa afya kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuhakikisha afya za Wananchi zinaimarika.
Ndg. Msovela ametoa pongezi hizo leo Mei 7, 2025 katika maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani
yaliyofanyika Kimkoa katika viwanja vya Kashauriri Mpanda Mjini.
Mbali na pongezi hizo pia amewaahidi Wauguzi wote Mkoa wa Katavi kuwa Serikali ya Mkoa
itayafanyia kazi malalamiko yao waliyowasilisha kwake ili Wauguzi waendelee kuwa na molali ya kufanya kazi.
Kwa upande mwingine, Chama cha Wauguzi (TANNA) Mkoa wa Katavi wameadhimisha siku ya Wauguzi Duaniani
kwa kutoa zawadi kwa Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.
Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani Kimkoa yamefanyika leo Mei 7, 2025 na Mgeni rasmi
alikuwa ni Mkuu wa Mkoa aliyewakilishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Ndg. Albert G. Msovela
na kauli ya mwaka huu ni "Uuguzi nguvu ya mabadiliko Duniani".