Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

WAHUDUMU WA AFYA KATAVI RRH WAKIPEWA MAFUNZO YA NAMNA YA KUMUHUDUMIA MGONJWA WA FISTULA NA MSAMBA

Posted on: August 13th, 2025



Leo Agosti 14, 2025 kumetolewa mafunzo kwa Wahudumu wa afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi watakaoshiriki kwenye kambi ya Matibabu Bure ya Wagonjwa wa Fistula na Msamba.

Kambi ya Matibabu ya Fistula na Msamba imeanza leo Agosti 14, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi na inatarajiwa kumahitimishwa Agosti 22, 2025.

Kambi hiyo inaratibiwa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania (AOFST), Fistula Foundation na kushirikiana na Wizara ya Afya.