TAKUKURU WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATAVI RRH
Posted on: October 18th, 2025Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Oktoba 19, 2025 imekabidhi msaada wa vifaa tiba maalum kwa ajili ya watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Francis Chalamila amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya mchango kutoka kwa watumishi wa Taasisi hiyo kama njia ya kushiriki katika shughuli za kijamii na kuunga mkono juhudi za kimaendeleo katika Sekta ya afya.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dr. Jonathan Budenu ametoa shukrani zake kwa TAKUKURU kwa msaada huo muhimu akisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa njiti na kuboresha huduma za afya kwa watoto.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dr. Deogratias Banuba ameshukuru msaada huo na kuwaomba TAKUKURU waendelee kuwa na moyo huo huo wa utoaji kwani wanaokoa maisha ya watu wengi.
Vifaa vilivyotolewa ni Radiant Warmer na Phototherapy ambavyo ni muhimu kwa uangalizi wa karibu kwa watoto njiti hususani katika kudhibiti joto la mwili.





