Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

RMO NA MOI KATAVI RRH WAFANYA UPASUAJI WA KIBINGWA WA MIFUPA KWA KUWEKA VYUMA NA KUCHUKUA SEHEMU YA MFUPA NA KUHAMISHIA KWENYE MGUU

Posted on: July 23rd, 2025

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Jonathan Budenu na Mganga Mfawidhi wa Hospitali

 ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Deogratias Banuba leo July 24, 2025 wamefanya upasuaji

wa Kibingwa wa mifupa kwa kuweka vyuma na kuhamisha sehemu ya mfupa (Bone Graft)

 kwenye nyonga na kuhamishia kwenye mguu.

Mgonjwa huyo alipata ajali mwaka mmoja uliopita na alikuwa anapatiwa matibabu kwa Waganga wa kienyeji.

Katika Hospitali yetu tunatoa huduma za Kibingwa za upasuaji wa Mifupa, Karibu tukuhudumie.