Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

RC MRINDOKO AKABIDHI VYETI KWA WAFANYAKAZI HODARI KATAVI RRH

Posted on: April 28th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko leo Mei 1, 2025 

amewakabidhi Watumishi wawili kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi vyeti

vya Wafanyakazi Hodari kwa mwaka 2024/25.


Akikabidhi vyeti hivyo kwenye maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mhe. Mrindoko

 amewapongeza  na kuwaasa kuwa kupata vyeti hivyo iwe ni chachu kwa Watumishi wengi kufanya kazi kwa bidii.


Waliokabidhiwa vyeti hivyo ni Ndg. Joseph Shirahe kutoka Idara ya Famasi na Bi. Yusta Mwakanyamale kutoka Utawala.



Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Kashauriri

 na Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko.


Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee Viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki’.