MKURUGENZI MKAZI WA SHIRIKA LA WRAIR-DoD TANZANIA Dr. LAURA CHITTENDEN AITEMBELEA KATAVI RRH
Posted on: July 17th, 2025
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la WRAIR-DoD nchini Tanzania Dr. Laura Chittenden,
akiwa na timu ya wataalamu kutoka Shirika la HJFMRI Tanzania na Timu ya Afya
Mkoa wa Katavi wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi
na kuangalia Huduma za Maabara na zile za Tiba na Matunzo (CTC) zinavyofanya kazi.
Kwa upande mwingine Dr. Chittenden alipata fursa ya kushuhudia mafanikio
ya utekelezaji wa shughuli zinazofadhiliwa na Shirika la WRAIR-DoD na kutekelezwa na HJFMRI.