Madaktari Bingwa Wabobezi wa Watoto kutoka Hospitali ya Kanda Mbeya
Posted on: November 8th, 2023Madaktari Bingwa Wabobezi wa Watoto wachanga kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya
Mbeya waja mkoani Katavi kutoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo watoa huduma za afya kwa Watoto
Wachanga mkoani Katavi.
Akizungumzia ujio huo, Wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi mapema leo Novemba
07, 2023, Dr. Lazaro Mboma, Ambaye ni Bingwa Mbobezi wa Upasuaji wa watoto kutoka Hospitali ya Rufaa
ya Kanda ya Mbeya, Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 3 na ni kwa Watoa huduma wote wa Mkoa wa Katavi.
Kwa upande mwingine, Dr. Mboma ameupongeza Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kwa ubunifu wa
kutengeneza vitanda vya kulalia watoto wachanga {Baby Cots} huku akiahidi kuwa Hospitali ya Rufaa ya kanda
ya Mbeya itashirikiana kwa ukaribu katika mambo mbalimbali na Hospitali ya rufaa ya Katavi.