Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

KARIBU KATIBU MKUU

Posted on: February 28th, 2023

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DKT. SEIF SHEKALAGHE NA  NAIBU KATIBU MKUU  DKT. GRACE MAGEMBE WAPOKELEWA WIZARANI 


Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Afya wameshiriki kwenye hafla fupi ya kuwapokea Viongozi wapya wa Wizara ya Afya walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambao ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe. 


Hafla hiyo fupi imefanyika katika Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali, Mtumba Dodoma mara baada ya shughuli ya uapisho wa viongozi hao ulifanyika Ikulu Chamwino.


Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo Dkt. Seif Shekalaghe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuani na kumteua katika nafasi hiyo.


Dkt. Shekalaghe ameahidi utumishi uliobora na kuendelea kutekeleza kazi na majukumu yote ambayo yamekuwa yakiendelea ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuboresha zaidi Sekta ya Afya na upatikanaji wa huduma bora za afya nchini.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe naye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuani na kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano katika maendeleo ya Sekta ya Afya


https://www.instagram.com/p/CpNH4SoN5_u/?igshid=YmMyMTA2M2Y=