Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

KAMBI MAALUMU YA MADAKTARI BINGWA - KATAVI RRH TAR: 11-15 SEPTEMBA 2023

Posted on: September 5th, 2023

Madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamini Mkapa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi watafanya kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu kwa magonjwa yafuatayo:

 • Matibabu na uchunguzi wa magonjwa ya watoto ikiwemo moyo kwa watoto wenye viashiria.
 • Kuona wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya fahamu. Upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
 • Matatizo ya afya ya uzazi wajawazito wenye changamoto mbalimbali za uzazi
 • Magonjwa ya mfumo wa chakula
 • Wagonjwa wenye shida ya mfumo wa mkojo, nguvu za kiume na uzazi wa mwanaume
 • Magonjwa ya mifupa, maumivu sugu ya magoti na nyonga
 • Matatizo ya macho
 • Kufanya upasuaji wa mifupa salama
 • Matatizo ya masikio, Pua na Koo ikiwa ni pamoja na upasuaji wake.
 • Kisukari, shinikizo la damu na kiharusi
 • Uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya figo

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kuchunguza na kupata matibabu kwa utaratibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kuanzia tarehe: 11 – 15/09/2023