HUDUMA ZA UCHUJAJI DAMU ZAANZA RASMI KATAVI RRH
Posted on: February 24th, 2025
Huduma ya Uchujaji Damu {Dialysis) imeanza rasmi mwezi huu wa Februari 2025
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.
Akiongea katika Mahojiano yake na kituo cha Radio cha Mpanda FM, Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dr. Deogratias Banuba
amesema kuwa kuanza kwa huduma hiyo kutawasaidia sana wakazi wa Mkoa
wa Katavi na mikoa Jirani.
"Kipindi cha nyuma huduma hii ya Uchujaji Damu haikuwepo, Wakazi wa hapa Katavi iliwalazimu waende Hospitali za mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza ili waweze kupata huduma hii. Kwasasa tunawakaribisha watu wote wenye changamoto za Figo na ambao wameanza tayari kupatiwa matibabu haya katika Hospitali za mikoa ya mbali waje kwetu kwani tunatoa huduma kwa wateja wote wa BIMA na CASH" Dr. Banuba.
Huduma hii ya uchujaji Damu ni mpya na ya kwanza katika Mkoa wa Katavi,
Na ujio wa Huduma hii ni moja ya maboresho makubwa yanayofanyika
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.
Ujio wa huduma hii ya uchujaji Damu haitasaidia tuu Wakazi wa Mkoa wa Katavi,
Bali itasaidia pia wakazi wa mikoa Jirani na Mkoa wa Katavi.