"Huduma ya m-mama imeokoa maisha Mama na Mtoto" Dkt. Grace Magembe
Posted on: July 13th, 2025
“Huduma ya M-mama imeendelea kuimarika siku hadi siku hasa katika kuokoa maisha ya mama na mtoto, hivyo imezaa matunda makubwa katika kuimarisha afya ngazi ya msingi,” amesema Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe Wikiendi iliyopita Jijini Dodoma wakati akitoa wasilisho kwenye Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri ulioratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.
Kupata huduma ya m-mama, Piga namba 115 bure kwa usafiri wa dharura wa mama na mtoto.
m-mama, Okoa Maisha. @wizara_afyatz @mmama_tz