H-MLELE FC WATOSHANA NGUVU NA KATAVI RRH FC
Posted on: June 14th, 2025
Timu ya Afya ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Mlele, H-Mlele FCl eo Juni 14, 2025 imetoshana nguvu dhidi ya Timu
ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Katavi RRH FC kwa kufungana goli 4-4.
Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja Mkuu wa Mpira wa Halmashauri ya Mlele ulishuhudiwa
H-Mlele FC wakiongoza goli 3-1 kipindi cha kwanza na baadae Katavi RRH FC
wakifanya 'Come-Back' kipindi cha pili na kupata matokeo ya goli 4-4.
Kwa matokeo hayo inakuwa ni muendelezo wa sare ya pili ya marudiano
dhidi ya Timu hizo mbili ambapo mchezo wa kwanza mwenyeji akiwa
Katavi RRH FC walitoshana nguvu kwa kufungana goli 2-2 .
#MichezoNiAfya