Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA KOMPYUTA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KATAVI

Posted on: August 18th, 2025

Benki ya NMB Tawi la Mpanda Mkoa wa Katavi leo Agosti 19, 2025 wametoa msaada wa Kompyuta Saba (7) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.


Akizungumza wakati akikabidhi Kompyuta hizo mbele ya Watumishi wa Hospitali, Meneja wa Tawi hilo, Ndg. Paul Gabriel Leseku amesema lengo la msaada huo ni kuwasaidia Madaktari na Wauguzi kufanya kazi kwa uharaka na ufanisi  katika kuwahudumia Wagonjwa.


Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dr. Deogratias Banuba ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa Kompyuta hizo na kuwaomba waendelee na moyo wa utoaji wasiishie tuu kwenye Kompyuta bali na misaada mingine pale panapohitajika.


"Niwapongeze NMB mmekuwa wadau wetu wakubwa pale ambapo tunapohitaji kushikwa mkono, Msaada huu kwetu ni mkubwa sana. Nawaomba tuendelee kushikana mkono na tusiishie hapa tu kwenye Kompyuta", amesema Dr. Banuba.