Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi
(Mpanda Hospitali)

RC MRINDOKO AZINDUA BASI LA WATUMISHI KATAVI RRH, ATOA PONGEZI KWA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Posted on: May 19th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko leo Mei 20, 2026 amezindua rasmi Basi la Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Akizungumza mbele ya Watumishi, Mhe. Mrindoko amesema Basi hilo litasaidia sana Watumishi kupunguza gharama za maisha kwa kuwarahisishia usafiri.

Kwa upande mwingine, Mhe. Mrindoko amewapongeza Watumishi wote wa Katavi RRH kwa kazi nzuri ya kutoa Huduma bora ya Kuwahudumia Wananchi.

"Mimi tangu hii Hospitali ianzishwe hapa Katavi sijawahi kutoka nje ya Mkoa kwenda kutibiwa, Huwa nakuja hapa kupata matibabu kwasababu huduma ni nzuri na kuna kila aina ya matibabu hapa. Niwapongeze sana KRRH." Amesema Mhe. Mrindoko.

Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dr. Deogratias Banuba amesema wazo la kununua Basi hilo Dogo aina ya TATA alilipata tangu mwaka jana 2025 na lengo lilikuwa kuwarahisishia usafiri Watumishi ili kuwahi kazini na pia kutumiwa kwenye matukio ya kijamii.