KATAVI RRH DAY KUFANYIKA FEBRUARI 14, 2026
Posted on: February 6th, 2026Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi anawakaribisha Wananchi
wote wa Mkoa wa Katavi kushiriki katika Wiki ya maadhimisho ya KRRH DAY
(Siku ya kuanzishwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi).
Maadhimisho haya yatatanguliwa na wiki ya utoaji huduma na uchunguzi wa afya BURE kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi katika maeneo yafuatayo: Uchunguzi wa saratani ya matiti, Saratani ya shingo ya kizazi, Tezi dume, Uoni hafifu na viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza(Presha & Sukari).
Huduma hizi zitaanza kutolewa Jumatano Februari 11 hadi Ijumaa Februari 13, 2026.





