Ukaribisho
Dr. Deogratias Gosbert Banuba
Mganga Mfawidhi
Karibu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi Hospitali yetu ipo Rungwa kata ya Kazima katika manispaa ya Mpanda.Hospitali yetu hutoa huduma mbalimbali pamoja na huduma za kibingwa kama ifuatavyo,Huduma za Mifupa,upasuaji mkubwa,Magonjwa ya ndani,huduma ya watoto,huduma za Mama na Mtoto,Afya ya Kinya na Meno,Tiba ya viungo saidizi,pamoja na huduma za kibingwa pia tunatoa huduma za chanjo ambazo ni chanjo ya homa ya Ini (Hepatitis B Vaccine) na chanjo ya homa ya manjano (Yellow fever vaccin ).Katika Hospitali yetu tunayo Maabara kubwa na ya kisasa kabisa inayotoa huduma mbalimbali .Hospitali yetu ina Huduma ya bima na huduma ya kulipia papo kwa papo na pia tunazingatia sera ya Afya ya Taifa kwa kutoa huduma kwa makundi maalumu.
Karibu tukuhudumie.